Ticker

6/recent/ticker-posts

Idadi ya walimu 'wapiga ulabu' wakati wa kazi na baada ya kazi yapungua Nachingwea.Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Imeelezwa kwamba idadi ya walimu walevi imepungua kwa kiasi kikubwa wilayani Nachingwea, mkoa wa Lindi.


Hayo yameelezwa jana mjini Nachingwea na mwenyekiti wa wilaya ya Nachingwea wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT), mwalimu Yonas Rashid alipozungumza na Muungwana Blog.


Mwalimu Yonas alisema CWT wilayani humu kimefanyanao vikao walimu mara kadhaa ili kushauriana nao na kuwakumbusha wajibu wao kwa mujibu wa ajira zao.


Kiongozi huyo wa chama cha walimu  amesema matokeo ya vikao hivyo nikupungua kwa idadi ya walimu walevi. 


Yonas alitaja sababu nyingine ya kupungua kwa kasi ya ulevi kwa walimu ni madiliko na tofauti ya tabia ya walimu wa sasa na walimu wa zamani.


Alibainisha kwamba walimu wa sasa wengi wao ni vijana ambao wana malengo na mitazamo ya maendeleo kulingana na wakati huu wa sayansi na teknolojia.


" Idadi kubwa ya walimu ambao walikuwa na tabia hiyo wamestahafu. Waliobaki ni vijana, wao wana mitazamo na malengo tofauti na hao walio watangulia," alisisitiza Yonas.


Alisema idadi ya walimu walevi imepungua kwa takribani asilimia tisini. Huku akitoa wito kwa walimu waendelee kuchapa kazi kwa mujibu wa ajira na wazingatie miongozo ya kazi zao.


Post a Comment

0 Comments