KOMBE LA DUNIA QATAR 2022 NA MGUSO WA KIPEKEE KWA WATANZANIA

Mwanzoni mwa mwaka huu unaoelekea ukingoni,Wakati ikielezwa namna Kombe la FIFA la Dunia kwa mwaka huu wa 2022 litakuwa na msisimko wa thamani,wengi walikuwa na maswali kadhaa yaliyohitaji majibu.


Ikiwa zimetimia takribani wiki 2 na siku kadhaa tangu michuano hii kuanza kutimu vumbi huko Qatar maswali haya kutoka kwa mashabiki wengi wa soka yanathibitika kujibiwa na kiu inakatwa.


Ubunifu wa kimandhari…teknolojia ya kushangaza, matokeo ya kustaajabisha ikijumuisha Taifa la Japan kuwachalaza vigogo wa soka kutoka bara ulaya, Ujerumani na Hispania. Bila kusahau mataifa ya Ubelgiji na Ujerumani kuaga mashindano katika hatua ya kampuni...


Yote haya yameongeza nafasi na ladha ya kunako Kombe la Dunia mwaka huu. Habari njema zaidi kwa watanzania mwaka huu ni ukweli na uhakika kwamba shindano hili kubwa zaidi duniani limekuwa likiruka LIVE na muonekano wa HD kupitia chaneli ya taifa TBC kupitia vyombo vyake bora vya Tbc1, Tbc Taifa, Tbc Fm na Tbc Online. 


Inafurahisha sana kusikia sauti ya furaha na vifijo kwa watanzania katika vyombo vya usafiri,maeneo ya biashara,makazi na hata taasisi za huku juu ya shindano hili wote wakitumia chombo cha Taifa TBC,


Watazamaji wa soka Tanzania wana mengi ya kufurahia juu ya hili, shukrani kwa TBC kwa kupata haki za maonyesho haya bure (FTA), mijini na vijijini hivi sasa kuna furaha juu ya Kombe la Dunia Qatar-2022.


Chaneli hii ya Taifa inapatikana bure kwenye visimbuzi vya aina zote, yaani vya malipo na vile vya bure hapa nchini.


Kwa kutumia Startimes Tanzania na Azam Tv ambao wanaruhusa kusambaza matangazo ya TBC bure kote Tanzania, hili Shirika la Taifa limekata kiu linaendelea kutimiza ahadi yake ya kuwapatia burudani takribani michezo 28 ya michuano hii kupitia TBC1 michezo yote 64 ya mashindano ya watanzania kupitia. TBC Taifa na TBC Fm (matangazo ya redio).


TBC1 inapatikana katika chaneli namba 101 katika Antena na chaneli namba 445 kupitia Dishi ndani ya kisimbuzi cha Startimes, kisimbuzi chenye wengine zaidi nchini.


Post a Comment

0 Comments