https://monetag.com/?ref_id=TTIb Rais wa zamani asema watawala lazima wazingatie matakwa ya waandamanaji | Muungwana BLOG

Rais wa zamani asema watawala lazima wazingatie matakwa ya waandamanaji

 


Rais wa zamani wa Iran ametoa hadharani maoni nadra akiwasifu waandamanaji wanaoipinga serikali na kuwataka wenye mamlaka kuzingatia matakwa yao "kabla hawajachelewa".


Mohammad Khatami, mwenye umri wa miaka 79, alisema "kauli mbiu nzuri" ya "mwanamke, maisha, uhuru" inaonyesha jamii ya Iraniinaelekea kwenye mustakabali bora.


Pia alikosoa kukamatwa kwa wanafunzi katika msako wa vikosi vya usalama.


Maoni hayo yalikuja katika taarifa ya kuadhimisha Siku ya Wanafunzi Jumatano.


Wanafunzi wamekuwa mstari wa mbele katika machafuko yaliyoanza katikati ya mwezi wa Septemba kufuatia kifo cha Mahsa Amini, mwanamke mwenye umri wa miaka 22 ambaye alizuiliwa na polisi wa maadili kwa madai ya kukiuka sheria ya vazi la hijabu.


Maandamano hayo yanayoongozwa na wanawake yameenea katika miji zaidi ya 150 na vyuo vikuu 140 katika majimbo yote 31 ya nchi hiyo na yanaonekana kuwa moja ya changamoto kubwa zaidi kwa Jamhuri ya Kiislamu tangu mapinduzi ya 1979.


Uongozi wa Iran, akiwemo Rais mwenye misimamo mikali Ebrahim Raisi, umezitaja kuwa ni "machafuko" yanayochochewa na maadui wa kigeni wa nchi hiyo na kuviamuru vikosi vya usalama "kukabiliana nao kwa uthabiti".


Kufikia sasa, waandamanaji wasiopungua 473 wameuawa na 18,215 wamezuiliwa, wakiwemo wanafunzi 586, kulingana na Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Kibinadamu (HRANA). Pia imeripoti vifo vya maafisa 61wa usalama.

Post a Comment

0 Comments