Russia kuuzia Pakistan mafuta kwa bei nafuu



Pakistan imesema Jumatatu kwamba Russia imeamua kuiuzia mafuta ghafi, petroli pamoja na dizeli kwa bei nafuu.


Naibu waziri wa mafuta wa taifa hilo la kusini mwa Asia Musadik Malik, amesema hayo katika mkutano na wanahabari mjini Islamabad baada ya kufanya mazungumzo na wenzake wa Russia wiki iliyopita mjini Moscow.


Malik ameongeza kusema kwamba ujumbe wa Russia ukiongozwa na waziri wa nishati utazuru Pakistan mwezi ujao, ili kukamilisha utiaji saini mkataba huo. Hata hivyo hakutoa taarifa za kina kuhusu ni lini hilo litakapoanza kutekelezwa wala viwango vya bei ya bidhaa hizo kutoka Russia.


Waziri huyo ameongeza kusema kwamba mazungumzo yao yalikuwa na mafanikio kuliko ilivyotarajiwa, akisema kuwa ni kwa ajili ya maslahi ya Pakistan, wakati inapojaribu kukabiliana na uhaba mkubwa wa mafuta kote nchini.

Post a Comment

0 Comments