VIDEO: Raia wa Iran afukuzwa nchini adaiwa kupanga njama za uhalifu


Idara ya Uhamiaji Tanzania imemuondoa nchini raia wa Iran, Hamidreza Mohammad Abraheh baada ya kumtuhumu kupanga na kuendesha vitendo vya kuhatarisha usalama wa nchi.

Raia hiyo ambaye amekaa nchini kwa zaidi ya miezi sita amedaiwa kutoa taarifa za uongo wakati akiomba visa jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya Uhamiaji sura ya 54.

Hayo yamebainishwa leo Desemba 6, 2022 na Kamishna wa Uhamiaji Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka Nchini, Samwel Mahirane wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema raia huyo amesaidiana na baadhi ya Watanzania kufanya ulaghai ndani ya Mamlaka hiyo akidanganya apatiwe visa ya kuishi hapa nchini kwa madai ameoa Mtanzania.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Post a Comment

0 Comments