https://monetag.com/?ref_id=TTIb Waasi wa M23 waunga mkono harakati za kuleta amani DR Congo | Muungwana BLOG

Waasi wa M23 waunga mkono harakati za kuleta amani DR Congo


Waasi wa M23, moja ya makundi makuu yanayopigana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamesema wako tayari kujiondoa katika maeneo ambayo wanayashikilia katika eneo hilo, kwa kuzingatia maazimio ya mkutano wa kilele wa mwezi uliopita uliofanyika mji mkuu wa Angola, Luanda


Kundi hilo la waasi limechukua maeneo mengi ya Rutshuru na Nyiragongo katika miezi ya hivi karibuni na kusababisha maelfu ya watu kulazimika kuyahama makazi yao.


Kundi la M23 pia limeomba kukutana na Jeshi la Kanda ya Afrika Mashariki pamoja na wasuluhishi wa mchakato wa amani unaoongozwa na viongozi wa kanda hiyo.


Taarifa kutoka kwa msemaji wa kisiasa wa M23 Lawrence Kanyuka, inaongeza kuwa kundi hilo linaunga mkono juhudi za kikanda kuelekea na suluhu ya kudumu la kuleta utulivu mashariki mwa DR Congo.


Haya yanajiri wakati ambapo mazungumzo ya amani ya wiki nzima yalihitimishwa Jumanne katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.


M23 hawakuwa sehemu ya mkutano huo, ambao uliwaleta pamoja wawakilishi kutoka kwa makundi 50 yenye silaha yanayofanya kazi katika eneo hilo lenye utajiri wa madini.


Wajumbe walikubaliana juu ya kupokonywa silaha na mpango wa kuleta utulivu kwa waasi wa zamani.

Post a Comment

0 Comments