Wamorocco wafurika mijini kushangilia ushindi wa kihistoria wa Kombe la Dunia

 



Mashabiki wenye furaha walimiminika katika mitaa ya miji mikubwa ya Morocco baada ya nchi hiyo kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.


Simba ya Atlas iliifunga Uhispania kwa mabao 3-0 katika mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare tasa.


Watamenyana na Ureno Jumamosi (15:00 GMT).


"Haiwezekani sio Morocco," ndivyo Shirikisho la Soka la Morocco lilivyoelezea ushindi huo.


Fataki zilipigwa na bendera kupeperushwa katika mitaa ya mji mkuu, Rabat, huku watu wakishangilia kwa kuimba na kupiga ngoma hadi usiku wa manane.

Post a Comment

0 Comments