Wanandoa wafariki kwa ajali Bukoba



Wanandoa wawili Tumaini John (41) aliyekuwa hakimu wa mahakama ya mwanzo Maruku katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba, na mme wake Geofrey John (42) mfanyabiashara, wamefariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kugongana na basi la kampuni ya Happy Nation.


Kamanda wa polisi mkoani Kagera  William Mwampaghale amesema kuwa ajali hiyo ilitokea Novemba 06, 2022  saa 5:30 asubuhi katika barabara itokayo Bukoba kwenda Biharamulo eneo la Ijuganyondo


Amesema basi hilo aina ya Youtong liligongana na pikipiki hiyo aina ya SANLG na kusababisha vifo vya watu hao


"Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva mmoja wa pikipiki aliyekuwa amepakia magunia ya mkaa kuisukuma pikipiki waliyokuwa wamepanda watu hao na kusababisha pikipiki yao kukosa mwelekeo na hivyo kugongana na basi hilo la Happy Nation, na kusababisha vifo vyao papo hapo" amesema Mwampaghale.


Post a Comment

0 Comments