Mahujaji 15 wa Nigeria wauawa na watu wenye silaha nchini Burkina Faso

 


Takriban Mahujaji 15 wakiislamu raia wa Nigeria waliokuwa wanaelekea Senegal waliuawa wakati watu wenye silaha nchini Burkina Faso walipolishambulia basi liilokuwa likiwasafirisha, ofisi ya rais wa Nigeria imesema Jumatatu.


“Rais Muhammadu Buhari amepokea taarifa za kusikitisha za mauaji hayo,” Ikulu ya Nigeria imesema katika taarifa bila kutoa idadi ya waliopoteza maisha au maelezo zaidi kuhusu shambulio hilo.


Msemaji wa ofisi ya rais wa Nigeria ameiambia Reuters kupitia ujumbe wa WhatsApp kwamba idadi ya waliokufa ni 15 kufikia sasa.


Kulingana na mamlaka ya kidini ya Senegal, washambuliaji wasiojulikana waliushambulia msafara wa mabasi Jumatano wiki iliyopita na kuua abiria 18.


Mahujaji hao walikuwa njiani kuelekea kwenye hafla ya kidini nchini Senegal, wakitokea Niger na Nigeria, safari ambayo inalazimu kuvuka ngome za wanamgambo wa kiislamu kaskazini mwa Burkina Faso na katikati mwa Mali.

Post a Comment

0 Comments