https://monetag.com/?ref_id=TTIb Zaidi ya 100 wauawa katika shambulio Nigeria- Wanakijiji | Muungwana BLOG

Zaidi ya 100 wauawa katika shambulio Nigeria- Wanakijiji


 Zaidi ya watu 100 wameuawa baada ya wanamgambo kushambulia kijiji chao kaskazini mwa Nigeria, wakaazi wanasema, ingawa serikali ya jimbo hilo inasema idadi kamili haijulikani. Mashahidi waliambia BBC News Hausa kumekuwa na "zaidi ya saa 48 za mapigano" kati ya walinzi na "majambazi" tangu Alhamisi wiki iliyopita.


Ilifanyika katika eneo la Bakori, jimbo la Katsina, na maafisa huko walitangaza uchunguzi siku ya Ijumaa na kutuma ujumbe kuwatembelea wanakijiji wanaoomboleza siku ya Jumapili.


Hata hivyo licha ya kuitaja hali hiyo kuwa ya kusikitisha, Katibu wa Jimbo la Katsina Alhaji Muntari Lawal anasemekana kuwaambia wakazi "wasingojee serikali" lakini wawe "jasiri vya kutosha kukabiliana na shetani kabla hawajawamaliza".

Post a Comment

0 Comments