https://monetag.com/?ref_id=TTIb Waziri Mkuu ataka nyumba zilizojengwa na serikali kuuzwa kwa bei nafuu | Muungwana BLOG

Waziri Mkuu ataka nyumba zilizojengwa na serikali kuuzwa kwa bei nafuu


Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amesema nyumba zote zinazojengwa na Taasisi za Umma katika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam zinapaswa kukamilika haraka ili ziuzwe ua kupangishwa kama ilivyokusudiwa.

Ameyasema hayo leo, Jumatano, Novemba 27 baada ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za NSSF, NHC na Watumishi Housing iliyopo katika Wilaya ya Kigamboni.

Waziri Mkuu amesema inasikitisha kuona kwamba watumishi wa umma na wananchi jijini Dar es Salaam hawana nyumba nzuri za kuishi wakati zipo nyumba nyingi nzuri zimejengwa na zinahitaji umaliziaji mdogo ili ziweze kukalika.

Aidha Waziri Mkuu ameitaka Menejimenti ya NSSF kakamilisha haraka ujenzi na uwekaji wa miundombinu ya umeme, maji safi na maji taka katika nyumba zake 161 zilizoko Tuangoma, 820 zilizoko Mtoni Kijichi na 439 zilizoko Dungu ili ziuzwe na kuepusha uwezekano wa uharibifu unaoweza kutokea kwa nyumba hizo kakaa muda mrefu bila kupata wanunuzi au wapangaji.

Ili kufanikisha jambo hilo Majaliwa amemtaka Mthamini Mkuu wa Serikali atathimini nyumba hizo na kutoa bei halisi ya soko kwa sasa ili kuwawezesha Watanzania wengi na husus