Feb 9, 2020

Tahadhari yatolewa dhidi ya ongezeko la maji katika ziwa Victoria

Bodi ya maji bonde la ziwa Victoria imewatahadharisha watumiaji wa maji katika ziwa hilo wakiwemo wavuvi pamoja na watumiaji wa vyombo vya usafiri katika ziwa Victoria juu ya athari zinazoweza kujitokeza kufuatia ongozeko la usawa wa maji ziwani humo kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

Tahadhari hiyo imetolewa na mkurugenzi wa bodi ya maji bonde laziwa Victoria mhandisi Florence Mahay ambapo amesema kuwa usawa wa maji katika ziwa hilo umeongezeka mpaka kufikia 1134.22 mamsl ikiwa ni tofauti ya sentimeta tano ukilinganishwa na  usawa wa juu zaidi kuwahi kufikiwa ambao ulikuwa 1134.27 kwa kipimo hicho kwa mwaka 1965.

Aidha mhandisi Florence amesema kutokana na hali ya hewa katika bonde hilo kipindi cha masika huwa mwezi wa april mpaka mwezi mei hivyo kuna uwezekano wa usawa wa maji katika bonde hilo kuongezeka Zaidi.

Bodi ya maji bonde la ziwa Victoria imekuwa ikifuatilia usawa wa maji wa ziwa Victoria kwa muda wa takribani miaka 56 mpaka sasa kuanzia mwaka 1964 ambapo kumbukumbu ya taarifa za bodi hiyo zinaonyesha mwaka 2006 ndio mwaka uliokuwa na usawa wa chini kabisa kuwahi kufikiwa kwa kuwa na usawa wa 11.31.87 
KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger