IGP Sirro hatutaki kutumia mabomu ya machozi kwenye uchaguzi mkuu



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema “Tunataka uchaguzi wa mwaka huu uwe ‘credible’, uchaguzi ambao ni wa haki kama Rais alivyosema. Hatutaki ifikie mahala tuanze kutumia mabomu ya machozi"

Amesema hayo akiwa kwenye ziara ya ukaguzi mkoani Singida ambapo amewataka Polisi kuendelea kushirikiana na wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuacha kujiingiza kwenye matukio ya uhalifu hususan wa kutumia silaha za moto

IGP Sirro amewataka Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na usalama za Wilaya na Mikoa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kwamba hadi kufikia sasa hali ya usalama nchini imeendelea kuwa shwari na kwamba matukio ya uhalifu yamepungua

Aidha, amewataka baadhi ya wananchi ambao ni washtakiwa au wafungwa wanaopata msamaha wa Rais kutoka gerezani, kuacha kujiingiza katika matukio ya uhalifu