Jul 19, 2020

Jimbo la Mtwara Mjini watia nia 48 wanaoenda kuchujwa

Na Faruku Ngonyani,Mtwara


Wakati zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwanaia Ubunge na Diwani ukikamilizika siku ya ijumaa tarehe 17 julai 2020, kwa jimbo la Mtwara Mjini watania nia waliochukua fomu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Ubunge wamefika 48.
Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha mapinuzi Mkoa wa Mtwara Selemani Sankwa amesema kuwa kwa idadi kubwa ya uchukuaji wa fomu kwa mwaka huu umetokana na matokeo na utendaji mzuri wa Serikali ya awamu tano inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DR,John Pombe Magufuli.
Aidha Sankwa amesema kuwa kwa jimbo la Mtwara Vijijini watia nia wamefikia 14, Jimbo la Nanyamba 5, Tandahaimba 15, Newala Mjini 15,Newala Vijijini 21,Masasi 18,Ndanda 15, Lulindi 21, Nanyumbu 17 ,ambapo jumla yao imefika watia nia 197 kwa upande wa majimbo.
Lakini pia kwa upande wa viti maalum wanawake waliochukua fomu wamefikian 38,viti maalum kwa upande wa vijana 7 na viti maalum kwa upande wa Wazazi wamefikia 2
Ikumbukwe mchakato wa kuwachuja watia nia hao utaanza tarehe 20 na 21 julai 2020 ambapo Halmshauri kuu chama cha Mapinduzi Taifa itaketi na kupiga kura za maoni na hatamae kamati za Siasa za Wilalaya na Sekretariet ya Mkoa mpaka taifa.
Attachments area

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger