Jul 3, 2020

Mgonjwa mwingine apandikizwa figo Hosp. ya Benjamin Mkapa

  Muungwana Blog 3       Jul 3, 2020

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), imefanikiwa kwa mara nyingine kupandikiza figo, ikiwatumia madaktari bingwa wa hapa nchini.

Hayo yamebainika wakati Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akiwa na jopo la wataalamu wa BMH na wale wa UDOM, walipoeleza mafanikio waliyoyapata kwa mgonjwa mwingine aliyepandikiziwa figo, na hali yake ikiendelea vizuri, pamoja na yule aliyetoa figo.

Pamoja na kupatikana kwa mafanikio hayo, lakini Dkt. Chandika akawa na wito mahususi kwa wananchi kujenga tabia ya kuchunguza afya zao, ili kuziokoa figo zisifike hatua ya kufa na kufanyiwa matibabu ya kusafishwa damu (Dialysis) au kupandikizwa figo (Transplant).
logoblog

Thanks for reading Mgonjwa mwingine apandikizwa figo Hosp. ya Benjamin Mkapa

Previous
« Prev Post