Jul 19, 2020

Uchebe avunja ukimya kuhusu Shilole


Uchebe amefunguka hilo baada ya kutukanwa na kushambuliwa mitandaoni kuhusu kusambaa kwa picha ambazo zilionyesha amempiga mke wake Shilole ambapo mwenyewe ameeleza kuwa,
"Naweza nikasema kwamba siwezi nikampa mtu faida ya kidunia kwa sababu hata nikimuomba pepo hawezi kunipa, kwa hiyo vitu vingine mimi kama mwanaume ambaye nilikuwa kwenye mahusiano ya ndoa iliyohalalishwa na Mungu siwezi nikamfaidisha mtu wa nje ila ikifika wakati nitazungumza ila kwa sasa hivi sina lolote la kusema, hakuna kitu kibaya kama mambo ya siri ukayaweka bayana" ameeleza Uchebe.
Ikumbukwe tu wiki moja iliyopita Shilole alipost picha kwenye mtandao wa Instagram zikimuonyesha ana damu na alama usoni mwake na kueleza kwamba huwa anapigwa na Uchebe.
KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger