Aug 2, 2020

Idadi ya maambukizi ya COVID-19 kwa Afrika Kusini yavuka 500,000

  Muungwana Blog 2       Aug 2, 2020
Nchini Afrika Kusini idadi ya watu wanaougua COVID -19 imepindukia 500,000. idadi hiyo ikiwakilisha zaidi ya asilimia 50 ya maambukizi yote ambayo yameripotiwa katika mataifa 54 barani Afrika.

Usiku wa Jumamosi, Waziri wa Afya Zwelini Mkhize alitangaza kuwepo maambukizi mapya 10,107. Afrika Kusini sasa ina jumla ya watu laki tano na tatu waliomabukizwa virusi vya corona, watu 8,153 wamefariki kutokana na COVID -19.

Taifa hilo lenye jumla ya watu milioni 58, linashika nafasi ya tano duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi, ikiwa nyuma ya Marekani, Brazil, Urusi na India.

logoblog

Thanks for reading Idadi ya maambukizi ya COVID-19 kwa Afrika Kusini yavuka 500,000

Previous
« Prev Post