Wasimaminzi Uchaguzi 2020 Majimbo ya Mikoa ya Lindi na Mtwara wapigwa msasa


Na Faruku Ngonyani, Mtwara
Kuelekea uchaguzi Mkuu Tarehe 28 Oktoba 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini (NEC) imeendesha mafunzo kwa Wasiaminzi na waratibu wa  Majimbo ya Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Kamishna wa Tume ya Taifa ya  Uchaguzi Asina Abirahi Omari amesema kuwa kutoa mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi ni jukumu la kikatiba Tume kwa  kuhakikisha watendaji hao wanapata namna bora ya matumizi ya vifaa kuelekea uchaguzi Mkuu Tarehe 28 Octoba 2020.

Aidha kamishina huyo ameongeza kuwa mafunzo hayo kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara yamewahusisha  waratibu wa uchaguzi Mkoa ,Wasimaminzi wasaidizi wa Uchaguzi ,Wasimaminzi wa Uchaguzi Jimbo ,Maofisa uchaguzi Wilaya pamoja na Maafisa Ugavi Wilaya.

Mafunzo hayo yateendeshwa kwa muda wa siku Tatu ili watendaji walioteuliwa juu usimaminzi wa Uchaguzi huo waweze kutambua mchakato mzima ili Uchaguzi  usiingiwe na dosari yeyote.

Uchaguzi Mkuu hapa Nchini unatarajia kufanyika Tarehe 28 Oktoba mwaka huu 2020 ambapo wananchi watapa fursa ya kuwachagua Madiwani ,Wabunge pamoja na Urais.