Aug 2, 2020

Zaidi ya watu 80 wamekufa kwa kunywa pombe haramu

  Muungwana Blog 2       Aug 2, 2020
Zaidi ya watu 80 wamefariki dunia katika siku za hivi karibuni kutokana na kunywa kilevi chenye sumu huko katika jimbo la Punjab nchini India.

Ripoti zaidi zinasema vifo hivyo vimetokea katika wilaya tatu za jimbo hilo la kaskazini na polisi imefanikiwa kuwatia mbaroni watu 25.

Kwa mujibu wa shirika moja kubwa la habari nchini India PTI, mamia ya watu wanapoteza maisha kila mwaka nchini humo kutokana na kunywa vilevi vyenye sumu ambavyo vinatengenezwa kinyume cha sheria na kuuzwa kwa bei nafuu ya Rupia 10 za India ambazo ni sawa na senti 13 za dola ya Marekani.

logoblog

Thanks for reading Zaidi ya watu 80 wamekufa kwa kunywa pombe haramu

Previous
« Prev Post