Oct 15, 2020

Ditopile, Ndejembi kama kawa, watinga kata ya Msamalo kutafuta ushindi wa CCM

  Muungwana Blog       Oct 15, 2020

 


Mpaka kieleweke! Ndiyo kauli waliyoitumia wagombea Ubunge, Deo Ndejembi wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma na Mariam Ditopile wa Viti Maalum Wanawake ambapo wamewataka wanachama na wananchi wa Kata ya Msamalo kijiji cha Mgunga na Kitongoji cha Ifunda na Mgondo kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi Oktoba 28 kumchagua Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge wa Chamwino, Deo Ndejembi ili walete maendeleo kwa kasi kwenye Jimbo hilo yatakayoendana na hadhi ya kuwa jimbo la Ikulu.


Wagombea hao wa Ubunge wamefanya mikutano miwili ndani ya kata hiyo ambapo mmoja wamefanya katika kitongoji cha Mgondo na Ifunda na mwingine wamefanya katika kijiji cha Mgunda ambapo wamemuombea kura Dk Magufuli, Ndejembi mwenyewe huku wakiwashukuru wananchi kwa kumpitisha, Elias Kaweya kuwa Diwani bila kupingwa.


Akizungumza katika mikutano hiyo, Ndejembi amewaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua yeye na Dk Magufuli kwa kura nyingi za kishindo ili waweze kuwatumikia na kuwaletea maendeleo kwa kasi kubwa.


" Ni lazima tumlipe Dk Magufuli upendo ambao ameuonesha kwa kuhamishia serikali Dodoma lakini zaidi yeye mwenyewe kuhamia Ikulu ya Chamwino, kitendo cha yeye binafsi kuhamia jimboni kwetu ni faida kubwa sana za kimaendeleo kwa sababu sasa hili haliwi tu jimbo la Chamwino bali makazi ya Rais, niombeni mjitokeze kwa wingi Oktoba 28 mkamchague awe mtumishi wetu wa kushughulika na kero zetu za Maji, Elimu, Barabara na Afya.


Mimi ni kijana wetu mnanifahamu, 2015 nilikuja hapa kura hazikutosha, mwaka huu Chama kimeniamini kikanipa ridhaa, kama ambavyo nimekua nanyi kwa miaka mitano nikiwa siyo Mbunge na nimeweza kushughulika na changamoto zenu ikiwemo kuwezesha kupatikana Milioni 60 za Ujenzi wa Sekondari ya Msamalo basi aminini nikiwa mbunge nitafanya zaidi ya hayo," Ndejembi.


Kwa upande Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake, Mariam Ditopile amesema miaka mitano ya Dk Magufuli imekua ya neeema kwa wananchi wa Chamwino na watanzania kwa ujumla na hivyo kuwaomba wamchague tena yeye na Ndejembi ili kwa pamoja washirikiane kusukuma maendeleo katika jimbo hilo ili liendane na hadhi ya Ikulu.


" Kwa ngazi ya Urais kinachoendelea sasa ni mashindano ya kila Wilaya kutaka kuongoza kwa kura za Rais Magufuli, Wilaya ya Chamwino ndio anapoishi Rais wetu itakua jambo la ajabu kama hatutompigia kura za kishindo Rais ambaye ametuletea Hospitali ya Uhuru yenye hadhi ya kisasa katika Wilaya yetu ili imalize adha yetu ya kusafiri kwenda Dodoma Mjini.


Katika vijiji ambavyo vimenufika na serikali ya Magufuli kwenye umeme ni nyie watu wa Mgunga na Kata ya Msamalo, niwaombe sasa mna Mbunge kijana mwenye nguvu na akili, mwenye connection ambaye ataweza kuwaharakishia maendeleo, mnalopaswa nyie kufanya ni kumpa kura nyingi yeye na Dk Magufuli Oktoba 28," Amesema Ditopile.


Nae Diwani mteule wa kata hiyo, Elias Kaweya amewashukuru wananchi wa kata hiyo kwa imani kubwa waliyompatia ya kumpitisha bila kupinga huku akiahidi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kushirikiana na mbunge wake katika kuwatumikia wananchi wa Msamalo.

logoblog

Thanks for reading Ditopile, Ndejembi kama kawa, watinga kata ya Msamalo kutafuta ushindi wa CCM

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment