Polisi akamatwa kwa kuwashambulia waandamanaji Nigeria



Maafisa katika mji wa kibiashara nchini Nigeria ambao wamewakamata polisi waliowashambulia waandamanaji wanaoendelea kuandamana dhidi ya ukatili wa polisi.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa polisi walifyatua risasi katika kundi la waandamanaji katika eneo la Surulere mjini humo.

Gavana wa jimbo la Lagos, Babajide Sanwo-Olu, aliwataja majina polisi hao wanne ambao amesema wanakabiliwa na kesi ya nidhamu:

Gavana Sanwo-Olu pia amesema kwamba jimbo limetenga naira milioni 200 (dola 521,000) kwa ajili ya kufidia waathiriwa wa ukatili wa polisi.

Serikali ya kitaifa imepiga marufuku maandamano katika mji mkuu, ili kutekeleza maadili ya kukabiliana na Covid-19.

Maandamano dhidi ya ukatili wa polisi yamefanyika katika miji yote nchini Nigeria katika kipindi cha wiki iliyopita.

Maandandamano yameendelea licha ya kuvunjwa kwa kikosi tatacha polisi kinachotuhumiwa kwa ukatili wa raia maarufu kama (Sars).




Post a Comment

0 Comments