Afrika yafanikiwa kupata dozi milioni 270 za chanjo ya corona

 

Umoja wa Afrika umenunua dozi milioni 270 za chanjo ya corona ili kusambaza barani Afrika.

Dozi zote zitatumika mwaka huu, alihaidi mwenyekiti wa AU rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

Idadi hii ni nyongeza ya dozi milioni 600 ambazo zilikuwa zimehaidiwa tayari ambazo bado hazitoshi kutoa chanjo kwa bara zima la Afrika.

Kuna wasiwasi kuwa nchi maskini zitachelewa kupata chanjo tofauti na mataifa tajiri.

Ingawa idadi ya maambukizi na vifo vinavyotokana na virusi vya corona viko chini katika mataifa mengi ya Afrika ukilinganisha na maeneo mengine duniani.

Aina mpya ya virusi vya corona nchini Afrika Kusini inashtua na kuongeza idadi ya maambukizi.

"Kutokana na jitihada zetu tumeweza kupata chanjo milioni 270 kutoka makampuni makubwa matatu yanayosambaza chanjo hiyo: Pfizer, AstraZeneca (kupitia taasisi ya Serum ya India) na Johnson & Johnson," Rais Ramaphosa alisema Jumatano.

Dozi zipatazo milioni 50 zitakuepo kuanzia kipindi kigumu cha mwezi Aprili mpaka Juni 2021," alisema.

Kwa kuongezea , bara hili la Afrika linatarajiwa kupata dozi 600 za chanjo ambazo zilitolewa kutoka Covax effort ambazo nimelenga mataifa ya kipato cha chini.

Lakini maofisa bado wanasubiri ufafanuzi zaidi na sasa wanafurahi kuwa wamepata suluhisho la mbadala, Nicaise Ndembi, mkuu wa ushauri wa sayansi kutoka kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika alisema.

Bwana Ramaphosa alisema maafisa wana hofu kuwa dozi kutoka Covax effort zitatolewa mwanzoni mwa mwaka 2021 na zitakuwa zinatosha kwa ajili ya wafanyakazi wa afya peke yake.

Kwa idadi ya watu bilioni 1.3 na kila mmoja akiwa anahitaji chanjo mbili ,Afrika inahitaji dozi zipatazo bilioni 2.6 ili kila mmoja apate chanjo yake.

Afrika imerikodi zaidi ya maambukizi milioni tatu ya virusi vya corona na vifo vipatavyo 75,000 . Ukilinganisha na Marekani ambapo kumeripotiwa kuwa na maambukizi yapatayo milioni 23 na zaidi ya vifo 383,000 vilivyotokana na corona.

Kumekuwa na haraka duniani kote katika kununua chanjo, huku nchi tajiri zikitajwa kununua chanjo karibu zote.

Post a Comment

0 Comments