Biden azindua mpango wa uokozi wa dola trilioni 1.9


Rais mteule wa Marekani, Joe Biden ameuzindua mpango wa uokozi wa dola trilioni 1.9 kwa ajili ya kupambana na janga la virusi vya corona na kuufufua uchumi. 

Akizungumza jana usiku Biden amesema masuala hayo mawili ni kipaumbele chake cha kwanza na kwamba hizo zitakuwa juhudi ngumu zaidi za kiutendaji ambazo wamewahi kufanya kama taifa. 

Amesema chanjo ya virusi vya corona inapaswa kutolewa ili kuwaokoa mamilioni ya Wamarekani. Mapema wiki hii, serikali ya Rais Donald Trump ilitangaza kuwa itatoa dozi zote za chanjo zilizopo. 

Wakati huo huo, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anataka hatua zaidi za haraka zichukuliwe kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona nchini humo. 

Hayo ameyaeleza jana wakati wa mkutano na maafisa wa ngazi ya juu wa chama chake cha Christian Democratic Union, CDU. Merkel amepanga kukutana na viongozi wa majimbo yote 16 wiki ijayo kuzungumzia vizuizi hivyo.

Post a Comment

0 Comments