Biden kuendeleza zuio la safari zilizoruhusiwa na Trump

Msemaji wa rais mteule Joe Biden'amesema Marekani itaendelea kuwa na sheria za kukataza watu kusafiri kutoka Uingereza, Uingereza, Ulaya na Brazil - licha ya rais Donald Trump kutangaza kuwa ameondoa zuio hilo.

Ikulu ya Marekani ilitoa agizo siku ya Jumatatu kuwa zuio la kuingia Marekani litamalizika Januari 26,siku sita tu baada ya bwana Biden kuingia madarakani.

Lakini msemaji wa Biden, Jen Psaki, alisema kwenye Twitter kuwa sasa si wakati wa kuondoa hatua hiyo ya watu kusafiri.

Bwana Biden anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumatano .

Marekani iliweka zuio la kusafiri kwa mataifa ya Ulaya mwaka jana mwezi Machi huku zuio kwa raia wa Brazil liliwekwa Mei.

"Kwa ushauri wa kikosi cha kitengo cha afya, mamlaka haina lengo la kuondoa zuio hilo Januari 26," aliandika kwenye twitter bi. Psaki, muda mfupi tu baada ya rais Trump kutoa tamko hilo.

"Ukweli ni kwamba tuna mpango wa kuimarisha hatua za kudhibiti maambukizi ya corona, na kuimarisha hatua za kiafya kwa wasafiri wa kimataifa."

Alisema kuwa hatari bado ni kubwa duniani kote hivyo huu si wakati wa kuondoa marufuku ya usafiri kimataifa.

Dakika chache kabla ya Ikulu ya Marekani kutoa tamko la rais Trump la kuondoa zuio la wasafiri wa Uingereza, na maeneo mbalimbali ya Ulaya. Taarifa hiyo haikuwaruhusa wasafiri kutoka China na Iran.

Kufuatia amri iliyotolewa na kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC), wasafiri wa ndege wanaoingia Marekani kuanzia Januari 26 watalazimika kuwa na cheti kinachodhibitisha kuwa hawana maambukizi ya corona ili kuzuia maambukizi kuingia.

Post a Comment

0 Comments