Maalim Seif: Misimamo ya vyama ya siasa kamwe isitumke kusababisha mifarakano na kuwagawa wananch wa Zanzibar


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad amesema misimamo ya vyama ya siasa kamwe isitumke kusababisha mifarakano na kuwagawa wananch wa Zanzibar.

Alisema jamii nyingi zimefarakana na kutengana kwa sababu za kuwa na misimamo tofauti ya kisiasa, na kuwataka wananchi kubadilika na kuendana na kasi ya serikal ya awamu ya nane katika kuwaunganisha wananchi kuleta maendeleo.

Maalim Seif aliyaeleza hayo huko Bibwini Mkoa wa kaskazini Unguj alipokuwa akizungumza na wazanzibar kwa lengo la kendeleza umoja uliopo Visiwani Zanzibar ambao umepelekea kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Alisema kabla ya mapinduzi wazanzibar waligawanyika kutoka na misimamo ya vyama vya Siasa na kuazia miaka ya 1992 watu walirejea tena huko.

“Mara baada ya Mapinduzi rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Aman Karume aliamua kutunga sharia mpya no 6/ 1964 ambayo ilikuwa na lengo la kuweka umoja wa wazanzibar” alisem Maalim Seif.

Alisema karume aliona Mbali kuleta sheria hiyo kuwaunganyisha wazanzibar.

“Kama sisi ni waumini wa mapinduzi kwa nini tusisimamishe umoja ambao uliasisiwa na wazee wetu tangu mwazoni mwa Mapinduzi” alisema Maalim Seif.

Aliwataka wazanzibar kutimiza wajibu wao katika kuendeleza Umoja na mshikamano kwa masilahi ya Vizazi vya leo na vinavyokuja.

Alisema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Husein Ali Hassan Mwinyi alikuwa na anahubiri umoja tangu wakati wa kampeni na mara baada ya kuapishwa alitimiza nia yake hiyo.

“Na Mara baada ya kuapishwa alinyoosha Mkono wa Maridhiano kwetu sisi(ACT Wazalendo) na kwa nini tusimpokee wakati tushamuona dhamira yake” alieleza Maalim Seif.

Alisema umoja na mshikamano katika nchi yoyote ile duniani ndio unaopelekea kupatikana Amani na kupelekea kuwepo maendeleo endelevu.

“Kama tuna migogoro watalii wala wawekezaji hawajii kwetu kwa hiyo umoja wetu tuuwendeleze na wala usiwe na mbadala wake katia kujenga Zanzibar yetu ili nchi yetu ipige hatua kimaendeleo” alisema Maalim Seif.

Alisema yeye akiwa kwenye kazi za makamu wa Kwanza wa Rais uwenyekiti wa ACT wazaledo anauweka Pembeni na kueleza kuwa kwanza ni Zanzibar mbele.

Kuafuatia kauli hiyo alimtaka Mku wa Mkoa wa Kaskazini Ungja Ayuob Muhammed Mahmoud kumchukulia hatua Sheha yeyote yule ambaye atafanyakazi zake kwa ubaguzi.

Alisema haiwezakani kiongozi wa Serikali ambaye ana mwakilisha Rais ambaye anapinga ubaguzi lakini Sheha akawa anafanya ubaguzi.

“Haiwezekani Rais anahimiza umoja na aridhiano lakini watokee wachache waaze kuturudisha nyuma lazima kiongozi kama huyo achukuliwe hatua” alieleza Maalim Seif.

Mapema Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Muhammed Mahmoud alimuhakikishia Makamu wa Kwanza kuwa mkoa wake unaunga mkono aslimia mia umoja wa kitaifa uliofikiwa.

Alisema kinachafanyika kwa sasa ni kuendeleza dhamira hiyo kila sehemu wanapokutana wananchi wa mkoa huo.

Kwa upande wao wanachi wa kaskazini Unguja walimuambia Maalim Seif kuwa wao hawa mashaka na umoja huo na kuwataka viongzi waw wakali anapotokea mtu kuaza kurudisha nyuma umoja huo.

“Makamu wetu wa Kwanza sisi hatuna shida na umoja wetu, lakini Masheikhe wetu wako ndani mwaka wa sababa, tunawaomba tujumuike nao” alisema Katibu wa Maimamu wa Mkoa huo, Salim Gharib Salim.

Imamu Salim alisema umoja huo ni furaha kwa hivyo kila mmoja anatakiwa kufurahi kwa hiyo ni vyema na na viongozi hao wa kidini na wao wafurahi.


Post a Comment

0 Comments