Mkutano wa UN kwa ajili ya kulinda sehemu za kidini


Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) limepitisha azimio la kulaani uharibifu wa sehemu za kidini na kudhamiria kufanya mkutano wa kimataifa juu ya ulinzi wa sehemu hizo.

Rais wa awamu ya 75 ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Volkan Bozkır, alisema kuwa uamuzi wa Saudi Arabia kufanya mkutano wa kimataifa unaoungwa mkono na Marekni pamoja na Jumuiya ya Ulaya, ulikubaliwa.

Ilielezwa kuwa mkutano huo utazingatia azimio la kulaani uharibifu wa sehemu za kidini na mashambulio ya kigaidi ya wanamgambo haramu ili kuzuia madhara na kulinda maadili.

Kufuatia uamuzi huo, iliarifiwa kwamba sehemu zote za kidini zina umuhimu mkubwa ulimwenguni wa kuwakilisha historia, muundo wa kijamii, mila na desturi kwa ujumla.

Uamuzi  uliopendekezwa na Saudi Arabia pia uliungwa mkono na nchi za Kiarabu zikiwemo Misri, Iraq, Jordan, Kuwait, Yemen, Bahrain, Sudan, Oman, Falme za Kiarabu na Palestina.


Post a Comment

0 Comments