Jan 23, 2021

Mwili wa Martha kuagwa leo Bungeni Dodoma


Mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum wa Manyara kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Martha Umbulla, utaagwa leo Januari 23, 2021, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Martha alifariki dunia usiku wa kuamkia Januari 21, 2021, nchini India katika hospitali ya HCG Mumbai, alipokwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Taarifa ya kifo chake ilitolewa na Spika wa Bunge la 12, Job Ndugai, na kueleza kuwa ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia itaratibu mipango yote ya mazishi.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, alituma salamu za rambirambi na kueleza jinsi gani alivyokuwa akimfahamu Martha, na kuongeza kuwa alikuwa ni mpole, mchapakazi na mpenda maendeleo.

Martha Umbulla, alizaliwa 10, 1955.KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger