https://monetag.com/?ref_id=TTIb Takukuru Manyara yampandisha Kortini mwenyekiti Mstaafu wa RIVACU kwa Uhujumu Uchumi | Muungwana BLOG

Takukuru Manyara yampandisha Kortini mwenyekiti Mstaafu wa RIVACU kwa Uhujumu Uchumi


Na John Walter-Manyara

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Manyara, Leo  January 15,2021 imemfikisha mahakamani aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa chama kikuu cha ushirika cha Rift Valley Cooperative Union (RIVACU)  Lohay Langay kwa tuhuma za uhujumu uchumi.

Shauri hilo namba 1 la mwaka 2021, limetajwa  katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara  mbele ya Hakimu Victor Kimario.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama, mwendesha mashtaka wa Takukuru mkoa wa Manyara Martin Makani,  amesema  Langay anatuhumiwa kufanya kosa hilo mjini Babati  Novemba 1 mwaka 2017 akiwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa RIVACU.

Makani amesema kwa uchunguzi uliofanywa na Takukuru, Langay akiwa Mwenyekiti wa RIVACU alijihusisha katika mkataba wa kikazi kwa kumpatia  ajira ya kuwa Mhasibu wa chama RIVACU, Paul Makoye bila idhini ya bodi ya wakurugenzi wa chama hicho cha ushirika ambapo katika kipindi chote cha ajira mtu Hugo  alijipatia shilingi Milioni sita na laki mbili.

Amesema kwa mujibu wa sheria ya vyama vya ushirika kifungu cha 134, kifungu kidogo cha (1) na cha (3) 14 na 16 ya jedwali ya ushrika sheria namba 6 ya mwaka 2013, inataka mtumishi au mtu yeyote alieajiriwa katika chama cha ushirika lazima ajira yake I we imethibitishwa na bodi ya wakurugenzi ambapo mtuhumiwa alitenda kinyume.

Makani amesema  kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na mambo kama hayo ni lazima akumbane na mkono wa sheria.

Post a Comment

0 Comments