https://monetag.com/?ref_id=TTIb Tetesi za soka kimataifa | Muungwana BLOG

Tetesi za soka kimataifa

 


Tottenham wamepanga kumhamisha mshambuliaji wa Southampton na England Danny Ings, 28. (Eurosport)

Meneja wa Southampton Ralph Hasenhuttl anasema hali ya kifedha ya klabu hiyo inamaanisha kuwa hawataweza kuongeza mshahara wa wachezaji muhimu kama vile Ings. (Mirror)

Ings anataka kurejea katika klabu ya Championi Ligi na anasubiri kwanza kusaini mkataba mpya na the Saints. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Inter Milan na Ubelgiji Romelu Lukaku, 27, hana haja ya kujiunga na Manchester City. (Express)

Liverpool na Tottenham wanaangalia uwezekano wa kufanya mkataba na kiungo wa kati wa Inter Milan Muitalia Nicolo Barella, 23. (Calciomercato)

Liverpool na Barcelona bado hawajakata tamaa ya kusaini mkataba na mlinzi wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28, licha ya kwamba Real Madrid wanakamilisha mkataba naye. (Sport1)

Manchester United wanaandaa dau la pauni milioni 11 kwa ajili ya mchezaji wa safu ya ulinzi ya Lens na Argentina Facundo Medina, 21. (La Voix du Nord - in French)

Nice wametuliza nia yao ya kumchukua kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28 kwa mkopo . (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli, 24, anaimani kuwa atasaini mkataba wake wa kuhamia Paris St-Germain katika kipindi cha dirisha la uhamisho mwezi Januari . (Sun)

Arsenal wameambiwa kuwa kiungo wa safu ya kati wa Argentine Emi Buendia, 24, ataondoka katika Norwich City wakati wa kipindi cha dirisha la uhamisho wa wachezaji. (Independent)

Manchester City wana chaguo la kumnunua tena mchezaji wa safu ya kati wa Aston Villa na Brazil, Douglas Luiz kwa pauni milioni 27.5 na muda wa chaguo hilo unakamilika msimu huu lakini meneja Pep Guardiola hatarajiwi kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka. (Birmingham Mail)

Montpellier wamekataa dau kutoka kwa West Ham kwa ajili ya mshambuliaji Mfaransa Gaetan Laborde, 26. (Guardian)

Atletico Madrid wanamtaka meneja Diego Simeone asaini mkataba mpya, utakaomuwezesha kubakia katika klabu hiyo hadi mwaka 2024. (AS - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Mnorway Martin Odegaard, 22, ameomba kuondoka katika klabu hiyo. (Marca)

Meneja wa West Ham David Moyes hatarajii kuongeza wachezaji zaidi katika kikosi chake mwezi Januari. (Evening Standard)

Mlinzi wa Newcastle Mmarekani DeAndre Yedlin, 27, anasema yuko gizani kuhusiana na hali yake ya siku zijazo kwani klabu hiyo bado haijafanya mazungumzo kuhusu mkataba wake. (Newcastle Chronicle)

Post a Comment

0 Comments