https://monetag.com/?ref_id=TTIb UN: Mataifa maskini yasaidiwe kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi | Muungwana BLOG

UN: Mataifa maskini yasaidiwe kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

 


Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP, limesema nusu ya ufadhili juu ya mabadiliko ya tabia nchi ulimwenguni, unapaswa kuelekezwa kwenye mataifa maskini ili kuyasaidia kukabiliana na ongezeko la joto duniani ambalo linasababisha maafa kama vile ukame, mafuriko na kuongezeka kwa kiwango cha maji baharini. 

Wanasayansi katika shirika hilo wamesema hali mbaya ya hewa iliyokuwepo mwaka jana ilisababisha mvua kubwa barani Afrika na kwamba kiwango cha juu cha joto na joto kali kwenye bahari ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi. 

Mwaka 2020 ulikumbwa na joto kali na hivyo serikali kote ulimwenguni zinahitajika zichukue hatua za kukabiliana na athari zaidi. 

Mkataba wa mazingira wa Paris wa mwaka 2015, unasisitiza kupunguzwa kiwango cha joto hadi chini ya nyuzi joto 2 kipimo cha Celsius.


Post a Comment

0 Comments