Feb 23, 2021

6 wafariki, 19 watekwa nyara katika Mashambulizi ya silaha Nigeria


Watu 6 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 19 kutekwa nyara kwenye mashambulizi ya silaha yaliyotekelezwa katika mikoa ya Kaduna na Katsina nchini Nigeria,.

Washambuliaji hao waliokuwa wakiendesha pikipiki waliendesha shambulizi la silaha katika wilaya ya Kajuru iliyoko mkoani Kaduna.

Watu 5 walipoteza maisha katika shambulizi hilo, na wengine 9 wakatekwa nyara huku nyumba nyingi zikichomwa moto.

Katika mkoa wa Katsina, mtu 1 alifariki kwenye shambulizi lililoendeshwa na watu waliojihami kwa silaha, ambapo wanawake 10 pia walitekwa nyara.

Vikosi vya usalama vilitumwa katika maeneo ya tukio na uchunguzi ulianzishwa kuhusu mashambulizi hayo.

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger