Chuma cha ajabu kilichoonekana DRC chateketezwa kwa moto


Chuma cha ajabu kilichoonekana katika eneo la makutano ya barabara jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimeteketezwa na moto kwa kuhofia uasili wa chuma hicho.

Watu mjini Kinshasa, wamekipiga mawe na kukichoma chuma hicho cha ajabu cha kung'aa chenye futi 12 ambacho kinafanana na vyuma kadhaa ambavyo vimekuwa vikionekana duniani kote miezi ya hivi karibuni, cha kwanza kilionekana Utah nchini Marekani mwezi Novemba mwaka jana.

Wengi walipokiona walianza kwa kukipiga picha na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, wengi walihofia imani za nguvu za giza.

"Tumeamka tu na kuona chuma hiki cha ajabu cha pembe nne... Tulishangazwa kwasababu ni chuma ambacho huwa tunakiona kwenye makala kuhusu freemasons au illuminati," mkazi mmoja wa eneo hilo Serge Ifulu aliiambia Reuters.

Uvumi kuhusu chuma hicho ambacho ulianza kusambaa katika mji wa Bandal mwishoni mwa wiki iliyopita lakini Jumatano wakaanza kukiteteza.

Post a Comment

0 Comments