Kembaki Kuuvaa Mfupa Uliowashinda Watangulizi Wake

 


Na Timothy Itembe Mara.

Mbunge wa jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki ameahidi kuushugulikia na kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Ardhi  uliodumu kwa mda mrefu baina ya JWTZ na Wananchi wa kata ya Nyamisangura.


Hatua hiyo ilikuja baada ya kupokea kero kutoka kwa wakazi wa maeneo hayo wakati akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua  utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi 2020-2025 ikiwemo kuwashukuru wananchi kwa kumchagua ili kuwa Mbunge wao.


Akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Bugosi,Diwani wa kata ya Nyamisangura,Thobias Elias Ghati  alisema kuwa leo tunakukabidhi mgogoro uliodumu kwa miaka (8) tangu tulipofanyiwa maeneo yetu tathimini na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa lengo la kutulipa fidia hadii sasa hatujalipwa na tumekwama kuendeleza maeneo hayo.


Ghati aliongeza kusema Wananchi wa ambao wanategemea maeneo hayo wanasumbuka hususani katika shuguli nzima ya uzalishaji kwasbabu maeneo hayo yana mgogoro na mtu akijaribu kwenda maeneo hayo anakumbana na mkono wa kipogo.


Naye Diwani kata ya Turwa Chacha Marwa Machugu Maarufu Chacha Musukuma alisema kuwa maeneo hayo ambayo kuna mgogoro na eneo lake lipo na kuwa yeye binafisi na wananchi kwa ujumla wameshindwa kuendeleza maeneo yao kwa kuheshimi Jeshi la Wananchi wa Tanzania9JWTZ) kwa sababu ndi wenye nchi pamoja na kusubiri utaratibu wa utatuzi wa mgogoro kisheria.


Musukuma alifafanua kuwa sheria ambayo hakuitaja niyamwaka gani alisema kuwa sheria hiyo inasema kuwa Mwananchi au eneo likifanyiwa tathimini ndani ya miezi sita halijafidiwa siku ya kulipa fidia kuna haja ya kulipa fidia ikiwemo na riba.


Pia Musukuma aliongeza kusema kuwa sheria hiyo ambaypo hakuitaja alisema kuwa sheria hiyo inasema kuwa endapo maeneo yaliyofanyiwa fidia hayajalipwa mwa miaka miwili kupita kuna haja sasa wamiliki wa maeneo hayo kuachiwa na wakaendeleza maeneo yao siovinginevyo.


Katika Ziara hiyo Kembaki alitembelea baadhi ya mashule na kukagua ujenzi na maendeleo kwa ujumla ambapo pia alipokea kero mbalimbali kutoka kwa wananchi ikiwemo ya uhaba wa madawa katika hospitali ya wilaya inayomilikiwa na halmashauri ya mji wa Tarime na kuwa watenda kazi wake hawahudumii wagonjwa ipasavyo.


Eliudi Mahiri ni moja ya wananchi waliotoa kero ambapo alimwambia Mbunge huyo kuwa baadhi ya Manesi na wahudumu wa hospitali hiyo wamejifanya kuwa Miungu watu wanatumia kauli chagfu kwa wagonjwa na ukiandikiwa dawa wanatoa kwa kuangalia sura vinginevyo unaambiwa nenda kanunue mitaani hapa kwetu hizo mdawa hatuna.

Post a Comment

0 Comments