Feb 23, 2021

Kenya kuandaa kura ya maamuzi kuhusu marekebisho ya katiba

 Kenya inatarajiwa kuandaa kura ya maamuzi kuhusu marekebisho ya katiba b
aada ya mswada wa Building Bridges Initiative (BBI) kuidhinishwa katika mabunge 24 kwa mujibu wa katiba.


Mabunge ya majimbo 10 zaidi yanajadili mswada huo kwa sasa na huenda idadi ya majimbo yanayounga mkono mchakato huo yakaongezeka.


Japo mswada wa BBI utahitajika kuidhinishwa na Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti kura ya maamuzi itafanyika hata mabunge hayo yasipouunga mkono.


Baadaye maspika wa mabunge hayo mawili watamfahamisha rais kuhusu uamuzi wao.

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger