Feb 27, 2021

Marekani iko tayari kufanya kazi bega kwa bega na Tanzania kuishinda Covid-19


Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umesema kuwa Marekani iko tayari kushirikiana na Tanzania kuzuia kusambaa kwa COVID-19, na kuishinda.


Katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao rasmi wa Ubalozi huo, Balozi wa Marekani nchini humo Dionald Wright amesema '' Ninataka kuzungumzia kuhusu Covid-19 na jinsi tunavyoweza kushirikiana kwa pamoja kuzuia kusambaa kwake na kutusaidia sisi sote kukaa salama''


Haya yanajiri baada ya Marekani kutoa tanagazo juma lililopita ikiwatahadharisha watu dhidi ya kusafiri nchini Tanzania kutokana na corona.


Hata hivyo hivi karibuni Tanzania imeonyesha kuimarisha juhudi za kukabiliana na virusi vya corona huku rais Magufuli akisema serikali yake haijamzuia mtu yeyote kuvaa barakoa.


Tamko hilo liliashiria kuwa Rais Magufuli amebadili msimamo wake kuhusu ugonjwa wa Covid 19.


Rais ailitoa wito kwa wananchi wenzake kuendelea kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona kama wanavyoelekezwa na wataalamu wa afya, akisisitiza kwamba serikali yake haijamzuia mtu yeyote kuvalia barakoa...Magufuli: 'Hatujazuia matumizi ya barakoa'


Tangu wakati huo viongozi na baadhi ya watu wamekua wakionekana kuchukua tahadhari hususan uvaaji wa barakoa na unawaji wa mikono.


Waziri anayehusika na masuala ya afya nchini Tanzania Dkt Doroth Gwajima Ijumaa kupitia tangazo lililotumwa mwenye mtanda wa Twitter wa Wizara ya anayoingoza aliwaomba viongozi na wananchi kushirikiana kuongeza kasi zaidi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.


Dkt Gwajima amekuwa akihimiza matumizi ya dawa za asili katika kukabiliana na magonjwa ya mfumo wa upumuaji

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger