Mkataba wa nyuklia wa Iran: Marekani iko wazi kwa pendekezo la mazungumzo 'wakati muhimu'


Marekani na nchi zenye uwezo barani ulaya zimetoa wito kwa Iran kurejelea utekelezaji wa nyuklia wa mwaka 2015.

Marekani imekubaliana na pendekezo la kushiriki katika mazungumzo yanayoihusisha Iran na nchi nyingine zenye ushawishi mkubwa duniani kwa lengo la kufufua mkataba wa nyuklia.

Iran iliapa kudhibiti mpango wake wa nyuklia kwa masharti ya kuondolewa vikwazo vya kiuchumi chini ya mkataba wa nyuklia wa 2015.

Lakini rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliiondoa Marekani katika mkataba huo mwaka 2018, hatua iliyoifanya Iran kuvunja ahadi zake.

Sasa Marekani imeonesha nia ya kujiunga tena na mkataba huo chini ya utawala wa Rais Joe Biden.

Siku ya Alhamisi, Utawala wa Biden umekariri ahadi yake ya kujadiliana na Iran kuhusu mkataba huo, unaofahamika kama Mpango wa pamoja wa kina wa utendaji- (JCPOA).

Msemaji wa idara ya mambo ya nje Ned Price amesema Marekani itaitikia mwaliko wa Muungano wa Ulaya EU, katika mazungumzo ya Iran.

Post a Comment

0 Comments