https://monetag.com/?ref_id=TTIb Shambulizi la silaha Mexico | Muungwana BLOG

Shambulizi la silaha Mexico

 


Watu 11 wameuawa na 2 kujeruhiwa katika shambulizi la silaha katika jimbo la Jalisco, Mexico.


Miili ya watu 11 imepatikana ndani na mbele ya nyumba, watu 2 waliojeruhiwa katika shambulizi hilo wamelazwa hospitalini.


Mnamo Februari 13, mifuko 18 iliyo na mabaki ya binadamu ilipatikana katika mji wa Zapopan wa jimbo hilo.


Kikundi cha madawa ya kulevya cha "Jalisco Next Generation" kinachofanya kazi katika jimbo la Jalisco kinajulikana kama kundi lenye nguvu zaidi katika mkoa huo.


Zaidi ya watu 300,000 wamepoteza maisha hadi sasa katika ghasia zilizosababishwa na vita ambavyo vilianzishwa dhidi ya wauzaji wa madawa huko Mexico mnamo 2006 bila mafanikio. Takriban watu elfu 40 walipotea katika kipindi ambacho zaidi ya watu 340,000 wa Mexico walihama makazi yao.


Jumla ya maiti 189 zilitambuliwa mwaka jana katika jiji la El Salto, katika jimbo la Jaliscoa.

Post a Comment

0 Comments