Feb 23, 2021

Umoja wa Ulaya wafikiria kuiwekea vikwazo zaidi Belarus

 


Umoja wa Ulaya huenda ukaiwekea vikwazo vingine zaidi Belarus baada ya serikali ya nchi hiyo kuwatia jela waandishi habari wawili kwa kitendo cha kuchukua vidio ya watu waliokuwa wakiandamana. 


Hayo yameripotiwa na shirika la habari la serikali la Poland PAP ambalo limemnukuu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Zbigniew Rau. 


Waziri huyo amenukuliwa akisema kwamba kwa bahati mbaya hali nchini Belarus imeendelea kudorora na kwamba idadi ya wafungwa wa kisiasa nchini humo imeongezeka kwa hivyo vikwazo zaidi huenda vikapitishwa dhidi ya nchi hiyo. 


Belarus inawashikilia zaidi ya watu 33,000 katika hatua zake za kutumia nguvu kuwaandama waandamanaji wanaoupinga utawala wa Rais Alexander Lukashenko, ulioingia madarakani kufuatia uchaguzi wa mwezi Agosti mwaka jana ambao matokeo yake yanapingwa na upinzani.

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger