Feb 23, 2021

Watu 28,000 wameathiriwa na mafuriko Indonesia


Watu 28,000 wameathiriwa na mafuriko katika eneo la Bekasi na Karawang katika jimbo la Java Magharibi mwa Indonesia.

Raditya Jati, mkuu wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Wakala wa Kitaifa cha Maafa, a amesema katika taarifa kwamba vijiji 4 vya Bekasi na vijiji 34 vya Karawang viliathiriwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa tangu wikendi.

Akitoa ripoti kwamba kiwango cha maji kimeongezeka hadi mita  2.5 katika baadhi ya mikoa, Jati amesema kuwa zaidi ya watu elfu 28 waliathiriwa na mafuriko, na kwamba uhamishaji wa watu 4,184 kwenda maeneo salama unaendelea.

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger