Watu 42 waachiwa huru na kundi la kujihami nchini Nigeria

 


Watu 42 nchini Nigeria wengi wao wakiwa watoto wameachiwa huru kutoka mikononi mwa kundi la kujihami lisilojulikana. Hata hivyo mamia ya vijana waliotekwa nyara bado hawajulikani walipo. 


Msemaji wa gavana wa jimbo la Niger, Mary Noel-Berje, ameliambia shirika la habari la Ujerumani, dpa kwamba walioachiwa huru walitekwa nyara kutoka kwenye shule iliyo karibu na mji wa Kagara katika eneo hilo. Wakati huo huo wasichana 317 waliotekwa nyara kutoka kwenye shule moja ya upili katika mji wa Jangebe, katika jimbo la Zamfara siku ya Ijumaa asubuhi pia bado hawajulikani walipo. 


Utekaji nyara unaofanywa na makundi ya kujihami umeongezeka nchini Nigeria katika miezi ya hivi karibuni. Wasichana na wanawake hulazimishwa kuolewa na wapiganaji au kuwa washambuliaji wa kujitoa muhanga huku wengine wakitumika kama vibarua.Aina nyingine ya utekaji nyara inafanywa na magenge ya wahalifu kwa nia ya kudai kulipwa fidia.

Post a Comment

0 Comments