Waziri Mhagama aagiza mfanyakazi aliyetimuliwa kurejeshwa kazini

 


Aliyekuwa mtunza stoo wa kampuni ya shamba la mkonge la Amboni Plantations (Kigombe Estate), Mwanaisha Mgunya amerejeshwa kazini na Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama bila kutarajia.


Hivi karibuni, Mwanaisha alipewa barua na ofisa raslimali watu wa kampuni hiyo ya kumuachisha kazi kwa madai kwamba utendaji kazi wake haukuwa na ufanisi kwenye kampuni hiyo.


Mwanaisha alipata ujasiri katika mkutano wa Waziri Mhagama uliofanyika Kigombe Estate na kumlalamikia kuwa hana cha kufanya na amekata tamaa ya maisha kwa sababu kampuni hiyo imemwachisha kazi bila kujali utumishi wake wa miaka 13.


Baada ya kusikiliza maelezo ya uongozi wa Kigombe Estate, Waziri Mhagama aliamuru Mwanaisha arejeshwe kazini leo leo kwa sababu sheria na taratibu za nchi hazikufuatwa wakati wa kumwachisha kazi.

Post a Comment

0 Comments