WHO: Ugonjwa wa Diphtheria ulisababisha vifo Yemen

 


Watu 116 walifariki mwaka 2020 kutokana na ugonjwa wa diphtheria nchini Yemen.


Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), lilitoa taarifa kwenye akaunti ya Twitter ya Ofisi ya Yemen, na kusema kwamba idadi ya watu wanaoshukiwa kuwa na ugonjwa wa diphtheria ilirekodiwa kuwa 1,425 mwaka jana, na watu 116 walifariki kutokana na ugonjwa huo.


Katika taarifa hiyo, ilielezwa kuwa WHO na serikali ya Japan zilipeleka dawa kwa wagonjwa 24,309 wa diphtheria na watu ambao waliokuwa kwenye mazingira ya maambukizi katika mikoa yote ya Yemen.


Maelfu ya watu walipoteza maisha katika mizozo ya Yemen.


Yemen ambayo ni moja ya nchi masikini ulimwenguni, inakabiliwa na shida kubwa zaidi ya kibinadamu ulimwenguni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambapo zaidi ya watu milioni 22 wanahitaji msaada na ulinzi.


Nchini ya Yemen, pia imekuwa moja ya eneo linalokumbwa na vifo vingi vya raia kama matokeo ya mizozo ya muda mrefu, uhaba wa maji safi, utapiamlo, upungufu wa dawa na vifaa vya matibabu na vile vile ukosefu wa huduma za kutosha za afya na kupelekea mlipuko wa magonjwa.

Post a Comment

0 Comments