Mar 3, 2021

Madaktari bingwa wafariki na kuacha simanzi Arusha

 


Jiji la Arusha, limekumbwa na simanzi kufuatia vifo vya madaktari bingwa wawili ambao ni maarufu katika jijini hapa, mmoja akiwa ni mmiliki wa hospitali ya St Thomas jijini Arusha.


Madaktari hao ni Dk Lamweli Henry Makando, mmoja wa wamiliki wa hospitali ya St Thomas ambaye alikuwa daktari bingwa na upasuaji na Dk Simon Kavavila daktari bingwa wa magonjwa ya watoto, wamefariki Jumatatu na Jumanne, baada ya kulazwa katika hospitali ya St Thomas na baadaye kukimbizwa hospitali ya KCMC.


Madaktari hao, wote walikuwa wakifanyakazi katika hospitali hiyo ya St. Thomas, lakini pia walikuwa wakitoa huduma katika hospitali nyingine, ikiwemo hospitali inayomilikiwa na kituo cha mikutano cha Arusha(AICC).


Akizungumza na mkurugenzi mwenza wa hospitali ya St Thomas, Dk Julius Msuya alisema kabla ya kufariki, madaktari hao walikuwa wamelazwa pamoja katika hospitali hiyo.


Alisema Dk Makando amefariki kutokana na changamoto za upumuaji.


"Tumepata pigo kubwa sana sio kwa hospitali tu, bali kwa wakazi wengi wa mkoa wa Arusha," alisema.


Alisema Dk Kavavila yeye alifariki hospitali ya KCMC baada ya kupelekwa kwa matibabu zaidi


"Taarifa za kina za Dk Kavavila unaweza kuzipata hospitali ya AICC ambayo alikuwa akifanya Kazi muda mwingi"alisema


Akizungumnzia vifo hivyo, mkazi wa Arusha, Neema Peter alisema kufariki kwa madaktari hao ni pigo kubwa kwani, katika jiji la Arusha walikuwa ni tegemeo kubwa kwa wagonjwa wengi.


"Hapa Arusha asilimia zaidi ya 60 ya watoto ambao walikuwa wanaugua walikuwa wanatibia na Dk Kavavila aliyekuwa anatoa huduma katika hospitali mbalimbali binafsi lakini pia kwa akina mama ambao walikuwa na matatizo ya upasuaji na magonjwa mengine walihudumiwa na Dk Makando," alisema.


Lenatus John, ambaye ni mwanafamlia wa Dl Makando,alisema msiba hupo nyumbani kwake eneo la Mushono na taratibu zitatolewa.


Wakati huo huo, Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha, Dk Widson Sichalwe alisema kifo cha madaktari hao kimesikitisha sana.

Wakati Mwenyekiti wa chama cha wasafirishaji wa abiria mkoa wa Arusha na Kilimanjaro, (AKIBOA), Locken Adolf alisema msiba huo ni mkubwa kwa Arusha kwani umewaondoa madaktari ambao ndio walikuwa wakiwasaidia.


"Dk Makando ni jirani yangu hapa Mushono tumepokea kwa masikitiko makubwa kwani amefariki akiwa anapambania afya za wengine," alisema.

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger