Mazungumzo ya Marekani na Qatar

 


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amefanya mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya nje wa Qatar Mohammed Bin Abdurrahman El Thani.


Msemaji wa Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price alitoa taarifa ya maandishi kuhusu mazungumzo hayo.


Taarifa hiyo ilisema, "Waziri Blinken alimpongeza Waziri mwenzake kwa mafanikio ya kihistoria katika Azimio la Al-Ula kati ya Qatar na Bahrain, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Misri kwenye Mkutano wa Baraza la Ushirikiano wa Ghuba (GCC).".


Akibainisha kwamba Blinken alimshukuru mwenzake kwa Qatar kukaribisha majeshi ya Marekani, Price alisema kuwa mawaziri hao wawili walijadili uungaji mkono wa Qatar kwa mazungumzo ya amani ya Afghanistan na umuhimu wa umoja katika ghuba.


Post a Comment

0 Comments