Mbunge CCM atoa magari ya wagonjwa

 


Mbunge wa Same Magharibi (CCM), Dk David Mathayo ametoa magari 10 ya wagonjwa kwa ajili ya kata 10 za jimbo hilo  lengo likiwa kuwezesha wananchi hasa wajawazito.


Akizungumza leo Alhamisi Machi 4, 2021 wakati wa kukabidhi magari hayo, Dk Mathayo amesema jimbo hilo lenye kata 20, kwa sasa ameanza na kata 10 akisisitiza magari mengine yanakuja kwa ajili ya kata nyingine.


"Ninatoa magari ya wagonjwa 10, leo nitakabidhi kwenye kata sita na kesho nitakamilisha kwenye hizo kata nyingine nne, nia yangu ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya na wanawahishwa hospitali pindi wanapohitaji huduma za haraka."


"Kwenye hili jimbo maeneo ya milimani wananchi hususani wajawazito wanapata wakati mgumu wanapohitaji huduma za haraka maana hakuna magari, na hili lilikuwa ombi lao kwangu, nimelitekeleza  nikiamini watasaidika na kumaliza vifo vilivyokuwa vikitokana na kuchelewa kufika vituo vya kutolea huduma,” amesema Dk Mathayo. 


Jasmini Juma mkazi wa kata hiyo amesema hospitali hiyo itawasaidia kuokoa vifo vya mama na mtoto.

Post a Comment

0 Comments