Mke wa mwanmfalme Harry , Meghan ashutumu kasri kwa 'kuendeleza uongo' dhidi yake

 

Mke wa mwanamfalme. Meghan Markle amesema kwamba Kasri la Buckingham haliwezi kutarajia yeye na mwanamfalme Harry kunyamaza iwapo linaendelea kusambaza madai ya uongo dhidi yake.


Katika kanda moja ya mahojiano na Oprah Winfrey , Meghan alikuwa ameulizwa alihisi vipi kuhusu kasri hilo kumsikia akisema ukweli , ''zungumza ukweli wako hii leo''. Meghan pia alisema kwamba: Iwapo hilo linakuja na hatari ya kupoteza vitu, nadhani kuna vingi ambavyo vimepotea tayari


Kasri la Buckingham linachunguza madai kwamba wawili hao walimnyanyasa mfanyakazi wa ufalme huo. madai ya unyanyasaji yaliowasilishwa dhidi ya Meghan yalichapishwa baada ya mahojiano na Winfrey kurekodiwa.


Mahojiano hayo na Winfrey ambayo yatapeperushwa moja kwa moja siku ya Jumapili nchini Marekani na siku ya Jumatatu nchini Uingereza , yanatarajiwa kuelezea utendakazi wa Harry na Meghan katika kipindi chao kifupi wakiwa wafanyakazi wa ufalme kabla ya kujiuzulu ili kwenda kuishi Marekani.


Katika kanda ya pili ya sauti iliotolewa na CBS, Winfrey anawauliza wafalme hao : Je munahisi vipi kasri la Buckingham likisikia mukizungumza ukweli hii leo?.


Meghan anajibu: Sijui jinsi wangelitarajia kwamba baada ya muda huo wote tungesalia kimya iwapo kuna mpango wa kasri hilo kusambaza uwongo kutuhusu. Wawili hao walijiondoa katika kazi zao kama wafalme mnamo mwezi Machi 2020 na sasa wanaishi California.


Ripoti moja katika gazeti la Times siku ya Jumatano ilidai kwamba mke huyo wa mfalme alipokea malalamishi wakati alipokuwa akifanya kazi ya ufalme huo.


Kulingana na habari hiyo, iliandikwa Oktoba 2018 wakati wawili hao walipokuwa wakiishi katika kasri la Kensington baada ya harusi yao iliofanyika mwezi Mei mwaka huo.


Barua pepe iliovuja iliotumwa na mfanyakazi mmoja, ambayo ilichapishwa na gazeti hilo, inadai kwamba Meghan aliwaondoa wasaidizi wawili kutoka katika jumba hilo.


#Ripoti hiyo pia iliongezea kwamba alikandamiza kujiamini kwa mfanyakazi wa tatu wa ufalme huo.

Post a Comment

0 Comments