Waziri Kalemani atoa miezi 9 kwa TANESCO ujenzi wa kituo cha kupozea umeme Simiyu kukamilika


Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, ametoa muda wa miezi tisa kuanzia sasa, kuhakikisha ujenzi wa kituo cha kupozea umeme kinachojengwa mkoa wa Simiyu, uwe umekamilika.

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Matogolo Kalemani, ametoa agizo hilo wakati wa uwekaji jiwe la msingi, katika ujenzi wa kituo cha kupozea umeme, unaojengwa eneo la Imalilo, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.

Mradi huo unaojengwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), unagharimu shilingi bilioni 75, ambazo ni fedha zinazotolewa na Serikali ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments