Zaidi ya watu 10 wauawa katika ghasia Myanmar

 


Kiasi cha waandamanaji kumi wameuawa leo wakati maafisa wa vikosi vya ulinzi nchini Myanmar walipotumia risasi za moto katika siku ya 30 ya maandamano kupinga hatua ya jeshi la nchi hiyo kuipindua serikali. 


Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti haya huku walioshuhudia wakielezea kupitia mitandao ya kijamii.Vituo 11 vya habari nchini Myanmar vilituma ujumbe kupitia mtandao wa Twitter kuhusu mamlaka kutumia gesi za kutoa machozi, mabomu ya kurusha kwa mkono na risasi za mipira dhidi ya waandamanaji katika mkuu, Yangon. 


Bado haijabainika idadi kamili ya vifo vilivyotokana na ghasia hizo. Siku ya Jumapili kulikuwa na ripoti ya vifo 18.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kuzungumzia suala hilo katika kikao cha faragha siku ya Ijumaa.Uamuzi huo umechukuliwa huku kukiwa na wito kutoka ndani ya Myanmar kwa Umoja wa Mataifa kutuma usaidizi.

Post a Comment

0 Comments