Apr 19, 2021

Dulla Makabila ahamia Simba "Hata kila shabiki wa Yanga anipe milioni sirudi ng'oo"

  Muungwana Blog 3       Apr 19, 2021


MSANII wa muziki wa Singeli kwenye ardhi ya Tanzania, Dulla Makabila amesema kuwa alikuwa ni shabiki wa Yanga kwa sababu familia yake aliikuta ikiwa upande huo jambo lililomfanya yeye pia awe shabiki wa timu hiyo.

Hivi karibuni Makabila aliomba kuwa shabiki wa timu ya Simba kwa kile alichoeleza kuwa ni maumivu aliyokuwa anayapata kutokana na matokeo ya timu hiyo aliyokuwa akiipenda awali.

Leo Aprili 19, Makabila ametambulishwa rasmi kuwa shabiki wa Simba na ameachia wimbo rasmi kwa ajili ya Simba. Unakuwa ni usajili mpya kwa upande mwingine kabisa ikiwa ni ule  wa mashabiki wa timu hiyo iliyo na tiketi ya kushiriki hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Makabila amesema:"Nilikuwa ninaipenda Yanga kwa kuwa niliikuta familia yangu ikiwa huko ila kutokana na maumivu ya matokeo ambayo yamekuwa yakipatikana nimeamua kuwa shabiki wa Simba kwa moyo wote,".

Haji Manara amesema kuwa Makabila atakuwa na jukumu la kuwa shabiki muaminifu wa Simba na atakuwa mtunzi wa nyimbo za Simba.

Wimbo wa leo amesema kuwa utatumika kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika..

logoblog

Thanks for reading Dulla Makabila ahamia Simba "Hata kila shabiki wa Yanga anipe milioni sirudi ng'oo"

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment