Fahamu kuhusu tatizo la tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu

 

Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.

Nini husababisha.
Tatizo ili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:
1. Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.

2. Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi kama maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k

3. Msongo wa mawazo na hasira.

4. Kula haraka haraka na kula unaongea.

5. Uvutaji wa Sigara

6. Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula asa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.


Jinsi ya kujitibu.

·         Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.

·         Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya Limao baada ya kula.

·         Tafuna mbegu za maboga zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula

·         Lalia ubavu wa kushoto na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.

·         Kunja miguu na ikalie uku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.

·         kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.

·         Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kuruka ruka.

·         Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi,.

·         Nenda hospitali kama tatizo ili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.

Post a Comment

0 Comments